Tarehe 25 may 2013 ni siku ya fainali ya ubingwa wa vilabu barani Ulaya ambapo Wajerumani Bayern Munich na Borrusia Dortmund zinakutana ktk fainali, pia Shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) litakuwa lina azimisha miaka 150 ya mashindano hayo ya klabu bingwa bara la Ulaya tangu yalipo anzishwa mwaka 1863, hii inakuwa ni fainali ya 150.
KWA NINI WAJERUMANI WAMEKUA BORA BARANI ULAYA
Bundesliga imekuwa ni ligi bora barani Ulaya ingawaje kitakwimu za UEFA bado iko nyuma kwa Spain (La Liga) ambayo inaongoza ikifuatiwa na England (Premier league). Ujerumani sasa imeanza kuvuna matunda iliyopandikiza miaka 14 iliyopita kwa kuacha wazawa tu ndio wachaguliwe kwenye timu yao ya Taifa na kuanza kukaribisha hata wahamiaji, pia kuwekeza kwenye soka la vijana. Dortmund ilitwaa ubingwa huo mwaka 1997 na Bayen ilikuwa nusu dakika kutwaa ubingwa huo mwaka 1999 walipofungwa na Manchester united, Timu ya Taifa ya Ujerumani ilitwaa Ubingwa wa Mataifa ya Ulaya mwaka 1996 nchini Uingereza na timu ambayo iliundwa na mchanganyiko wa wachezaji kutoka mataifa mengine na hasa Ulaya ya Mashariki. Matokeo hayo mazuri yalikuja baada Mpango mzuri wa makubalino ya malipo ya matangazo ya mechi za Ligi ya nchi hiyo uliofanywa kwa pamoja baina ya shirikisho la soka la nchi hiyo (DFB), Vilabu shiriki na kampuni ya TV mwaka 1992, uliwezesha vilabu vikubwa kuanza kulipwa pesa nyingi na kununua wachezaji wakubwa na wazuri kutoka nje ya Ujerumani na hivyo baada ya miaka mitano kuifanya Bundesliga kuanza kuwa na msisimko na ongezeko la wachezaji wa kulipwa nchini humo lilipanda mara mbili toka alsilimia 17 mpaka 34, na hiyo ilileta changamoto kwa wachezaji wa Kijerumani na Kocha wa Taifa wa nchi hiyo wakati huo BERTI VOGTS alichagua baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa wajerumani kiasili kama Sean Dundee asili yake toka South Africa, Paulo Rink mwenye asili ya Brazil, Kevin Kuranyi, Gerald Asamoah (Ghana). Sean Dundee aliumia mwaka 1997 na hakuwahi kurudi tena ktk kikosi cha Ujerumani kama.
Baada ya matokeo mabovu ya kombe la dunia mwaka 1998 ( Kwa kutolewa hatua za robo fainali na Croatia) na yale ya EURO 2000 ambambo pia walifungwa na Waingereza kwa mara ya kwanza ktk miaka 34, iliwashitua sana Wajerumani, Ndipo mwaka 1999 mwezi may Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la soka la nchi hiyo (DFB) FRANZ BECKENBAUER, Kocha wa Taifa aliye mrithi Berti Vogts wakati huo Mr ERICH RIBBECK na Mkuregenzi wa maendeleo ya Vijana wa DFB Mr DIETRICH WEISE wakaamua kuwekeza ktkt soka la vijana wa Kijerumani kwa kuweka Sheria vilabu vyote vinavyo shiriki ligi kubwa nchini humo kufungua academies na kuwa na timu za vijana na kuamuru vituo vyote 121 vya michezo nchini humo kuwasaidia vijana wa umri wa kuanzia miaka 10 mpaka 17 na mazoezi ya kiufundi, pia waliingilia kati sheria ya uhamiaji ambayo iliwanyima vijana wahamiaji kupewa nafasi ktkt vituo hivyo na kuwapendelea wazawa amtokeo ambayo yamezaa matunda na kuleta mafanikio makubwa ktk soka la nchi hiyo , vitua hivyo vilianza kutoa wachezaji kidogo kidogo na hasa wahamiaji walioingia moja kwa moja kwa timu za taifa za vijana mpaka kubwa , ODONKOR DAVID, DENNIS AOGO, LUKAS PADOLSK. MIROSLAV KLOSE,SEBASTIAN JUNG, CAUCAU, PIOTR TROCHWSKI, JEROME BOATENG SAMI KHEDIRA, MARKO MARIN, MESULT OZIL na wengineo udhamini wa vituo vya michezo vya kiserikali unafanywa kwa pamoja na makampuni ya .DEUTSCHE TELCOM. LUFTHANSA,ADIDAS,THE PAULANER BREWER, AUDI,COCA-COLA , SIEMENS, BURGER KING , CONTINENTAL NA SHERATON HOTELS, MERCEDES _ BENZ na VOLKSWAGEN
No comments:
Post a Comment